Ugunduzi Wangu Wa Ajabu Wa Uislamu

 

Wakati mtu aliniuliza hivi karibuni jinsi nilikuja katika kundi la Uislamu, mimi nilishangaa. Kwa maana mimi kamwe sikuwahi kuwa na mawazo ya kuja kwangu katika Uislamu kama kuwa hatua muhimu. Ni lini nilianza kuhoji Ukatoliki? Ni lini mimi nilitaka kuwa muislamu? Majibu ya maswali haya na mengineyo yanahitaji mafikira mengi kuliko nilivyofikiria. Ili niweze kujibu maswali haya, inabidi nianze mwanzo kabisa ndio muweze kuelewa mahali maisha ilikuwa imenifikisha hadi mwishowe nikaweza kukubali ukweli wa uislamu. Nilikuwa muislamu nikiwa na miaka 67, na nashukuru Mungu kwa kunibariki nikaweza kuwa mwaminifu wa uislamu.

“Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni. Namna hivi Mwenyezi Mungu anajaalia uchafu juu ya wasio amini.”

(Quran 6:125)

Nililelewa katika familia ya wakatoliki halisi, nikiwa msichana wa kati ya watoto watatu. Babangu alifanya kazi kwa bidii na kwa masaa marefu kila siku. Alikuwa anatoka mapema kila siku na kurudi usiku wa manane. Hii yote ilikuwa ndio mamangu aweze kukaa na sisi nyumbani akilea dada zangu na mimi. Siku moja ya kuhuzunisha sana, mamangu aituambia kwamba babangu alikuwa amepata ajali ya barabarani. Alifariki kighafla na maisha yetu ikageuka kabisa. Vile hayo mabadiliko yote yalikuwa yanafanyika, mamangu akatwambia lazima ingebidi arudi kufanya kazi. Mamangu ambaye alikuwa muuguzi alilazimika kurudi kazi ili aweze kutulea. Alipata kazi kwa hospitali iliyokuwa karibu, mara mingi akifanya mara mbili kwa siku. Lakini sasa na hii kazi mpya mamangu hakuweza kutuchunga kama alivyokuwa anatuchunga mbeleni. Ijapokuwa alitupeleka shule ya kikatoliki,kazi yake ilimzuia kuwa mwangalifu kwa watoto wake wa kike.

Kwa hivyo,nilipata wakati mwingi wa kupoteza na marafiki wangu kwa mahoteli yaliyokuwa karibu na nyumbani.Hapo ndipo nilipatana na mwanaume muislamu ambaye alikuwa mzuri na baadaye akawa mume wangu.Mamangu hakuwaijua kuwa mimi hushinda na huyu mwanaume.Nilipomwambia kuwa nina mpenzi na ningetaka kuolewa,alinionya kuwa mimi na huyo mwanaume tumetoka katika maisha mawili tofauti na baadaye tutakuwa na mashida.Alisema kama kutakuwa na watoto hapo baadaye katika maisha yetu,mashida kuhusu dini hayangekosa kuzuka.Nilikuwa miaka ishirini na singewai fikiria kuwa tungewai pata mashida katika ndoa yetu.Nilimpenda kwa dhati sana na nilikuwa na furaha kuwa kungekuwa na mtu ambaye angenichunga.Bwana yangu hakuwa anafuata dini sana na nilifikiri kua ningeweza kumbadilisha awe mkatoliki.Na kwa kuwa hatukuwa katika kiwango kimoja cha maisha,nilijiona kuwa na uwazi wa fikra na nilikuwa na furaha kuwa nachukua utamaduni mpya.Kila kitu kilionekana kuendelea vizuri kwa miaka kadha.Tulikuwa na furaha na swala la dini au utamaduni halikuwahi kuwa chanzo chetu cha matatizo.Mungu alitubariki na mwana wa kiume na miaka kadhaa baadaye alitubariki na mwana wa kike.Hata hivyo tuliendelea na maisha yetu na hata nikaanza kuenda na watoto wetu kanisani.Bwana yangu hakuwahi nikataza kuenda kanisani kila juma.Lakini baada ya kupeleka watoto wetu kanisani mara kadhaa,ndipo aliponiongelesha na kuniambia kuwa hataki nipeleke watoto kanisani.Kusema ukweli nilikasirika.”Lakini mbona,” Nikamuuliza,”kuwa katika dini lolote ni bora kuliko kukosa kuwa katika dini lolote,”Nilibishana.Sikuwahi elewa shida ilikuwa gani ya kuwapeleka kanisani.Kufikia hadi sasa hatujawai zungumzia swala la dini.Hata sijawai uliza kama kuna dini lingine isipokuwa dini la kikatoliki.Nilizaliwa kama mkatoliki na nilidhani kuwa kikatoliki ndio dini ya kweli.Kwa maelezo ambayo singeweza kuelewa kabisa,ilionekena kwamba kuanzia siku hiyo,matatizo mengi yalianza kujifichua.Tulibishana kila wakati-kuhusu kila kitu na kila mtu.Sasa vitu vidogo vinakuwa vikubwa.Dini likawa swala hasa la sisi kubishana.Utamaduni wetu tofauti ukawa swala pia la kubishana.Tulibishana kuhusu wakwe,na cha kuhuzunisha sana tulibishana kuhusu jinsi tutakavyo walea wetu.Kila kitu ambacho mama alituonya kuhusu kilikuja kuwa kweli.

Amani tu ambayo ilikuwa baina yetu ni hekima,ukweli,kujali na upendo ambayo baba ya bwana yangu,baba mkwe,alikuwa nayo na ndoa yetu.Baba mkwe alimpenda mtoto wake pamoja na wajukuu wake,lakini kwa dhati alinipenda kama binti yake.Alikuwa kidini na mcha Mungu muislamu na mwenye hekima.Kwa wakati huo,kwa kuwa sikuwa nimezungukwa na dini ya kiislamu,baba mkwe ndiye aliyekuwa wa kwanza kunianzisha kiislamu.Aliomba kila ombi,akafunga kila mwezi wa Ramadhani,na alikuwa mkarimu sana kwa maskini.Niliweza kuhisi uhusiano wake na Mungu.Kwa kweli,baba mkwe alikuwa mkarimu sana kwa maskini hadi kila siku akija nyumbani kutoka msikitini angemwita mtu mmoja maskini aje nyumbani wale chakula pamoja naye.Alifanya hivi kila siku.Hadi kufikia kifo chake akiwa miaka tisini na tano,jamaa zake wanamkumbuka kuwa na tabia hii.

Baba mkwe hakupendelea kubishana kwangu na mume wangu kwa hivyo alitupa ushauri nasaha kuwa tutafute ufumbuzi kabla watoto wetu wateseke juu ya kupigana kwetu.Alijaribu mno kutusaidia kupata ufumbuzi.Alimwonya mwanake kuwa anipee wakati nijaribu dini yangu,lakini haikuwa kuhusu dini pekee.Nilichanganyikiwa na nikaamua kuchukua mapumziko.Nilipomuuliza mume wangu tuwachane,aliitikia kuwa hilo ndilo uamuzi mzuri kwa ndoa yetu.Wajua msemo kuwa ”Kukosekana hufanya moyo kuwa na upendo.”Ila si kwa upande wetu.Hata ilifanya nyoyo zetu ziwe mbali kabisa.Baada ya kutengana,sisi wote tulitaka mgawanyo wa kudumu na tukaelewana kuwa tunataka talaka.Lakini nilitaka mno watoto wetu waishi nami,tulihisi kwamba itakuwa vyema watoto wakikaa na baba yao.Alikuwa na nafasi nzuri,kihela,kuwalea na kuwaburudisha;kitu ambacho sikuwa nimejitayarisha kuwapa.Niliwatamani kila usiku.Nilirudi kuishi na mamangu na nikaendelea kuwaona kila mwisho wa wiki.Mume wangu angewaleta watoto kila ijumaa wakati wa alasiri na angewachukua asubuhi mapema siku ya jumapili.Hata kama mpango huu uliniuma,ilikuwa bora kukosa nikose kuwaona.

Kila usiku kabla ya kuingia kitandani,ningesoma Bibilia.Watoto wangu walipokuja kuzuru,ningewasomea kifungu bila kujali kama wanaelewa au la.Baada ya kusoma kifungu,kila usiku niliomba usaidizi kwa Yesu na usiku huo mwingine kwa Malaika wa Mungu,na usiku huo mwingine kwa waumini tofauti,usiku unaofuatia kwa bikira Maria. Lakini usiku moja hatukuwa na mwengine yeyote wa kuomba usaidizi,waumini wote niliowajua walikwisha. Kwa hivyo nikajiambia ”Sasa tutamuomba Mungu.”Mwanangu wa kiume akaniuliza ”Sasa Mungu ni nani?” Nikasema ”Ni ule aliyekuumba na akaniumba. Yeye ndiye jirani wetu wa kweli na wa milele.” Akaanza kufikiria kuhusu maneno hayo.Kwa maelezo yangu,nikapapasa msalaba wangu tena. Nikasema ”Sasa mshukuru Mungu.”Akaangalia msalaba akasema ”Mama sasa huyu nani?” Nikasema ”Huyu ni Mungu. Yeye ndiye mwana wa Mungu.” Akasema ”Umeniambia tu dakika kidogo zilizoisha kuwa Mungu ni Milele.Itakuwa aje na huyu ameshakufa?” Sijawai kwa maisha yangu jua huo ukweli.Akaniuliza huyu Mungu huwa anatoka wapi? Nikamjibu kuwa alitoka kwenye tumbo la bikira Maria. Akasema,” Kumbe alizaliwa hapo mbeleni.” Nikasema ndio. Kisha akasema ”Lakini mama uliniambia kuwa yeye ni milele.Hakufi na hazaliwi.Mwana wangu wa kiume ambaye sasa alikuwa na miaka nane aliniuliza moja kwa moja ”Mama ,mbona usimuulize Mungu usaidizi?” Nilishangaa na ninakumbuka nilipatwa na mshtuko kuwa hata mwanangu anahoji dini yangu. Nikamwambia kuwa pia mimi huwa namuuliza Mungu.Sikuwaijua kuwa mwanangu atakuja kuwa mwiba mara kwa mara upande wangu,ambaye angekuwa ananikumbusha kuwa nafaa kumwabudu Mungu mmoja ambaye ni wa kweli.Asante Mungu.

Mwishowe, niliolewa tena na nikahamia Nchi ya Australia na mume wangu mpya.Mume wangu akapeleka familia yake Saudi Arabia.Nilitamani kuwaona watoto wangu na baadaye nilianza familia nyingine huko Italia na nikawa mama wa mabinti watatu.Bado,kila usiku niliomba ”Katika jina la Baba,la Mwana na la Roho Mtakatifu.” Miaka ilipita haraka. Nilipata msisimko majira moja;kuwa watoto wangu wa kiume na kike wangekuja kunitembelea.Vitu vingi vilinipita kichwani. kama, je wangefurahi kuniona baada ya kukosa kuonana kwa muda mrefu? je tungeongea kuhusu nini?Niliomba usaidizi.Hofu zangu zote zilipotea baada ya kuona watoto wangu katika uwanja wa ndege.Kulikuwa na dhamana ya papo kati ya mama na watoto wake na ilikuwa ni kama muda kidogo ilipita.Mwanagu wa kiume ndiye aliyeongea sana kati yao wawili.Alihakikisha kuwa ameniambia hao hawali nyama ya nguruwe na chakula ambazo zina pombe,tabia ambayo ilidumu toka wakati niliolewa na babake.Kwa divai,ilibidi niwache kupika nayo kwa wakati ule ambao wangekuwa kwangu.

Tulikuwa na majira nzuri,tukajuana,wao wakaja kujuana na madada wapya,kuenda ziara,kuogelea.Sikutaka wakati huu uishe.Lakini nilijua kwamba wana maisha yao huko Saudi Arabia na wangetaka kurudi.Nilimuuliza binti yangu swali nililoliogopa sana la vile wanavyohusiana na mama wa kambo.Nilifurahi aliponiambia kuwa anatunzwa kama binti yake.

Watoto wangu walinizuru mara mbili zingine wakati wa majira.Wakati mwanangu alifikisha miaka ishirini na moja,alikuja kuishi nami kwa miezi sita.Tungebishana kuhusu dini kwa kweli.Mimi na mwanangu tunalingana kiutu,lakini tuna tofauti zetu-na zile dhahiri pia!Mimi ni umoto wa hasira kwa migogoro,mwanangu ni mtulivu,hivyo yeye huelekea kudumisha hali ya utulivu wakati nimekasirika na mambo. Licha ya pambano hii,naamini ni kazi katika neema yetu na tunapata uwiano katika kujadiliana kwetu.Tunafanana sana kwa kuwa tuna upendo,ukarimu na watu wenye roho ya kusaidiana.Ninachothamini sana katika mwanangu ni kujitolea kwake katika kila kitu anachofanya.Yeye ni mnyenyekevu, mpole na ana maadili sana na analengo la kufikia chochote anachoweka katika akili yake na ninaheshimu hili.Ninathamini uwezo wake wa kuwa na akili nzuri kwa maswala tata.Ana umantiki na hatashindilia swala moja.Huwa anajaribu kutafuta jawabu katika maswala yote vyovyote awezavyo.Niliendelea kumuombea kuwa siku moja atabadilika awe mkatoliki. Nilitaka sana awe padri- nilijua atakuwa padri mzuri. Alikuwa kijana mzuri na aliye muogopa Mungu. Nilipomwambia angeweza kuwa padri mwema, mwanangu alitabasamu akaniambia, mamake angekuwa muislamu kwanza kabla yeye akuwe padri wa katoliki.

Baada ya miezi sita, mwanangu alisema anataka kuenda Amerika. Alifanikiwa kufika Amerika na akatengeneza makao Miami, Florida. Wakati huo huo mimi nilibaki nikawa mjane na binti mmoja nyumbani. Mwanangu alitaka sana niende nikae naye huko Amerika, sasa tukaenda na binti yangu huyo mmoja. Tulipenda sana Amerika na binti yangu akatengeneza maisha yake huko kwa haraka. Mimi na mwanangu tuliendelea kuongelelea kuhusu kikatoliki na uislamu lakini hakuna yeyote aliyekubali kubadilisha maoni yake. Saa zingine majadiliano kuhusu Trinity ilipoanza, sikupata jibu la kumwambia. Niliinua tu mikono na kutoka hapo. Nilikasirika kwa sababu niliona nikama ana shambulia dini langu.

“Mbona huwezi kuwa kama kila mtu mwingine?” Niliuliza. “Waislamu wengine hunikubali na huwa hawajaribu kunibadilisha. Siko kama kila mtu mwingine.” Akanijibu,”Nakupenda. Mimi ni mwana wako na nataka uende mbinguni.” Nilimwambia kwamba mimi bila shaka nitaenda mbinguni- mimi ni mwanamke mwema, mwenye hadanganyi, wala kuiba. Mwanangu akajibu,”Hizi vitu ni muhimu, na husaidia kwa hii maisha ya duniani. Lakini kwenye Quran imesema la kwamba mara mingi Mungu hasamehi ushirikina. Quran lasema kwamba dhambi moja ambalo Mungu hawezi samehe ni kumshirikisha, lakini atasamehe chochote kingine kwa mwenye anataka. Aliniomba nisome na nigundue uislamu. Vitabu vililetwa ili niweze kufungua akili, lakini nilikataa. Nilizaliwa mkatoliki na nitakufa mkatoliki.

Miaka kumi iliyofuata, niliishi karibu na mwanangu, na bibi yake na familia. Nilitamani lakini kuonana na binti yangu aliyekuwa bado anaishi Saudi Arabia. Haikuwa rahisi kupata visa. Mwanangu alisema na mzaha kwamba ningekubali tu uislamu,hiyo ndio ingekuwa visa yangu ya kuingia Saudi Arabia, kwa ajili ningeweza kupata umrah visa ( Hija makkah, Saudi Arabia visa) Nilimwambia kwa ukali ya kwamba sikuwa Muislamu. Baada ya kazi mingi, nilipata visa ya ugeni, kutembelea binti yangu, ambaye sasa alikuwa mama ya watoto watatu. Kabla niende, mwanangu alinikumbatia akaniambia vile alikuwa amenipenda na vile angetaka sana niweze kuenda mbinguni. Aliendelea kwa kusema vile aliweza kupata kila kitu alichotamani duniani isipokuwa tu mama aliye kuwa Muislamu. Aliniambia kwamba aliomba Mungu kila siku aweze kunibadilisha roho yangu nikubali uislamu. Nilimwambia hilo halitawahi fanyika.

Niltembelea Binti yangu Saudi Arabia na nikapenda sana Nchi hilo, na hali ya hewa, na watu wa huko. Sikuwa nataka kutoka baada ya miezi sita, ikabidi niombe ugani. Nilikuwa nasikia Adhan (kuitwa kwa maombi) mara tano kwa siku na ningeona waaminifu wakifunga maduka zao na kuenda kuomba. Ijapokuwa ilinigusa, niliendelea kusoma biblia kila asubuhi na jioni na mara mingi pia nilisema rozari. Hakuna siku yoyote yenye binti yangu ama muislamu yoyote mwingine aliwahi niongelesha kuhusu uislamu ama kujaribu kunibadilisha. Waliniheshimu na wakanikubalisha niendelee na dini langu.

Mwanangu alikuwa anakuja Saudi Arabia kunitembelea. Nilifurahi sana kwa sababu nilikuwa nimekaa sana bila kumuona. Vile tu alifika akaanza tena kuniongelesha kuhusu dini na umoja wa Mungu. Nilikasirika. Nikamwambia kwamba nilikuwa nimekaa Saudi Arabia mwaka mzima na hakuna aliyekuwa ameniongelesha kuhusu dini. Na yeye siku yake tu ya pili huku, alikuwa ameshaanza kunihubiria. Aliomba msamaha na akaniambia tena vile angetaka sana nikubali uislamu. Na mi nikamwambia tena sitawahi toka ukristo. Akaniuliza kuhusu Trinity na ningeweza aje kuamini kitu ambacho hakikuwa kina maana. Akanikumbusha ya kwamba pia mimi mwenyewe nilikuwa na maswali kuhusu haya. Nikamwambia ya kwamba si lazima kila kitu kiwe na maana – inabidi mtu tu awe na imani. Ilionekana ni kama alikubali hilo jibu, na nilifurahia kwamba nilikuwa nimeshinda mjadala wa dini. Aliniambia nimuelezee miujiza ya yesu. Nilidhani sasa tumeanza kuelewana. Nilimuelezea kuzaliwa kwa yesu, bikira Mary, na kukufa kwa Yesu kwa ajili ya dhambi zetu, Mungu kupumua roho yake ndani ya Yesu, Yesu kama Mungu, Yesu kama mwana wa Mungu. Alikuwa amenyamaza muda huo wote nilipokuwa nikiongea. Halafu akauliza,” Mama, kama Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu siku ya ijumaa, halafu kama ulivyosema, akafufuka baada ya siku tatu, nani aliyekuwa ana ongoza dunia siku hizo tatu? Mama, nielezee hayo.” Nilifikiria kuhusu hilo swali na saa hizo sikuweza kuona mantiki ya jibu lolote lililokuja kwa akili.

Nilisema,” Yesu ni mwana wa Mungu, Yesu na Mungu ni kitu kimoja.” Mwanangu akajibu, ” Ng’ombe wana ndama; ng’ombe wadogo. Paka wana kijipaka, paka wadogo. Binadamu wana watoto; binadamu wadogo. Mungu akiwa na mtoto, huyo ni nani? Mungu mdogo? Na kama ni hivyo, je inamaanisha uko na Mungu wawili?” Halafu akauliza, “Mama, wewe unaweza kuwa Mungu?” Nikamwambia hilo ni swali la ujinga. “Binadamu hawezi kuwa Mungu.”( sasa nilikuwa nimeanza kukasirika) Halafu akauliza, ”Yesu alikuwa binadamu?” Nikajibu, “Ndio.” Halafu akasema, “Kwa hivyo hawezi kuwa Mungu.” Kusema kwamba Mungu alikuwa binadamu ni mkanganyiko. Mungu hawezi kuwa kama binadamu kwa sababu itamaanisha muumbaji amekuwa kiumbe chake mwenyewe. Ndiyo aweze kuumbwa lazima kwamba akuwe hayupo, na kama hayupo, angeweza aje kuumba? Na tena kama aliumbwa, inamaanisha kwamba kulikuwa na mwanzo, kinyume na kuwa kwake milele. Kwa ufafanuzi, kiumbe kina haja ya muumba. Kwa sababu viumbe lazima ziwe na muumba. Mungu hawezi hitaji muumba kwa sababu yeye ndio muumba. Kwa hivyo kuna utata dhahiri katika swala hilo. Kudai kwamba Mungu alikuwa kiumbe chake ina maana kwamba alihitaji muumba. Ambayo ni dhana kejeli. Ni kinyume na dhana za msingi za Mungu kuwa hakuumbwa, na kwamba hakuhitaji muumba, na yeye ndiye muumba. Nilijua kwamba sikuwa na jibu la kumwambia, nikamjibu,” wacha nifikirie juu ya jibu.”

Hiyo jioni, nilifikiria kwa muda mrefu kuhusu kile mwanangu alikuwa amesema. Wazo la kuwa Yesu alikuwa mwana wa Mungu halikuwa na mantiki kwangu tena. Pia niliacha kukubali kwamba Yesu na Mungu walikuwa kitu moja. Kabla nilale hiyo siku, mwanangu aliniambia nimwombe Mungu na nimuulize yeye mwenyewe aniongoze kwenye njia sahihi. Niliahidi mwanangu kuwa ningeombea kwa dhati jibu kutoka kwa Mungu. Nilienda kwa chumba changu na nikasoma kitabu ambacho mwanangu alikuwa amenipatia. Halafu nikafungua Quran takatifu na nikaanza kusoma. Ilikuwa ni kama kitu ilikuwa imeinuliwa kutoka moyoni mwangu. Nilijihisi tofauti. Niliona ukweli kwenye uislamu. Sasa nilikuwa napigania nini hii miaka yote?

Usiku huo, niliomba Mungu peke yake‐ Sio Yesu, ama Mary, ama malaika, ama roho takatifu. Kwa Mungu peke yake na nikalia, na nikaombea uongozi. Niliomba kwamba kama uislamu ilikuwa chaguo sahihi, anibadilishe roho na akili. Nilienda kulala. Asubuhi ilipofika, nilitangazia mwanangu ya kwamba nilikuwa tayari kukubali uislamu. Alishtuka. Sisi wote tukaanza kulia. Binti yangu na mjukuu wakaitwa na kutazama kuwasilishwa kwa shahada yangu (Tamko la Uislamu la imani katika umoja wa Allah na kukubalika kwa Mohammed.( Amani na baraka za Allah ziwe juu Nabii wa Allah). Kama Nabii wa Mungu). Katika kiarabu, kiingereza, na Italian.

أشهد أن لا إله إلاَّ الله و أشهد أن محمد رسول الله
ASH-HADU ANLA ILAHA ILLA-ALLAH WA ASH-HADU ANNA MOHAMMADAN RASUL-ALLAH”.
“There is no God except Allah and Muhammad (PBUH) is His Messenger and Last Prophet.”
“Nakiri kuwa hakuna Mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe wake.”

Sikiliza video ya shahada

Shahada ni tamko la Uislamu la uaminifu wa umoja wa Allah na kukubali kwa Muhammed (Amani na baraka ziwe juu ya nabii wa Allah) kama Nabii wa Allah. Nilijihisi kama mwanamke tofauti. Nilikuwa na furaha ni kama mtu alikuwa ameondoa pazia la giza kutoka moyoni mwangu. Kila mtu aliyekuwa ananijua hakuwa anaamini ya kwamba nilikuwa nimebadili dini. Mimi mwenyewe sikuwa naamini. Lakini Uislamu ulikuwa unafanya nihisi sawa, nikiwa na amani.

Vile mwanangu alivyorudi Marekani, nilijifunza jinsi ya kusoma surah-al-Fatiha kwa kiarabu na sasa naweza kufanya maombi. Niliendelea na maisha yangu kama kawaida ijapokuwa sasa nilikuwa muislamu. Nilipenda sana kuhudhuria mikutano ya familia nikiwa na binti yangu na matukio ya kijamii pia. Ningehudhuria harusi za familia na marafiki, sherehe za hina, aqiqah( kukaribisha mtoto duniani), na mikutano iliyofanyika mtu alipofariki. Baada ya miezi sita ya kubadili kuwa muislamu, nilikuwa kwa mazishi yenye ilinigusa moyo na kuimarisha vile dini la uislamu llikuwa nzuri. Kijana mdogo alikuwa amefariki kwa ajili ya ugonjwa. Vile binti yangu alikuwa anajitayarisha kuondoka kwenda kutoa rambirambi, nilimuuliza kama alikuwa anajua familia hiyo vizuri. Alijibu kwamba hakuwa anawajua. “Mbona basi uende?” Nikamuuliza. ” Kwa sababu hiyo familia inaomboleza. Ni wajibu wangu kama muislamu kwenda na kutoa msaada wowote wenye naweza.” Niliamua kuvaa na kuenda na yeye. Nilienda pamoja na binti yangu kutoa rambirambi kwa familia ya kijana huyo na nilishangazwa na idadi ya watu waliokuwa wamehudhuria. Nilishangazwa na hilo jambo la watu hao wote kuweza kuja kupatia familia msaada. Kile tu nilikuwa naweza kufikiria nilipokuwa naangalia familia ikiomboleza, ni vile dini la uislamu ni nzuri hadi hao watu wote walikuwa wanahisi ni wajibu wao kupeana msaada. Tukio hilo moja, lenye waislamu walikuwa wanaonyesha huruma, lilionesha uzuri mwingine wa uislamu.

Nimekuwa muislamu kwa miaka minane sasa, Alhamdullilah. Tangu hizo siku, nimefanya Umrah mara mbili nikiwa na mwanangu na binti yangu. Mimi na mwanangu na binti yangu tulitembelea kabah (jijini la Mecca, Saudi Arabia.) Na Holy Prophet’s Mosque Madinah. Juzi tu nimesherehekea siku yangu ya kuzaliwa ya kufikisha miaka sabini na tano, Alhamdullilah. Saa zingine mi hufikiria kuhusu maumivu ya moyo niliyokuwa napatia mwanangu, lakini mwanangu alikuwa na furaha mingi sana kunitumikia na pia kunileta kwa dini la Islam. Alisema tena kwamba Nabii aliambia binadamu, “Peponi lipo chini ya miguu ya mama.”Maana ya hii hadithi ni kwamba unafaa kutumikia mamako, na umshughulikie vizuri. Ni kwa uhakika kwamba kwa kuwa kwa miguu yangu ndivyo kulikuwa na peponi ya sisi wawili. Pia nilikuwa najiuliza kama binti yangu pia angenifuatilia sana nibadilishe dini, kama ningekuwa nimekuwa muislamu mapema zaidi. Lakini mwanangu alinikumbusha kwamba Allah ni mpangaji bora kabisa, na ni yeye tu ambaye anaweza patia mtu Hidaya (mwongozo).

“Kwa hakika wewe humwongozi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoza amtakaye.”

(Quran 28:56)

Jambo bora lenye Allah alikuwa amenibariki nayo nikuniongoza kwa njia ya uislamu, na kunifanya niwe muislamu. Na inshallah tutaingia na mwanangu pamoja peponi.
« AMEEN »